Starboy ya The Weeknd yatabiriwa kuuza kopi zaidi ya 350k ndani ya wiki moja
Albamu mpya ya The Weeknd ‘Starboy’ inatabiriwa kuuza nakala 350k ndani ya wiki moja tangu ilipotoka Novemba 25.
Kwa mujibu wa HITS Daily Doublem, albamu hiyo yenye nyimbo 18 itauza kopi kati ya 350,000-400,000 ndani ya wiki moja.
Muimbaji huyo wa Marekani mwenye asili ya nchini Ethiopia aewashirikisha mastaa kadhaa kwenye albamu hiyo akiwemo Kendrick Lamar, Future na Lana Del Rey.
Kwa sasa albamu hiyo inashika namba tatu kwenye chati za Top 100 za Billboard.