Adam Mchomvu apanga kuishitaki kampuni ya simu
Mtangazaji wa Clouds Fm, Adam Mchomvu kaka Baba Jonii, amechukizwa na kitendo cha mtu anayejifanya mfanyakazi wa kampuni ya mtandao wa simu wa Tigo, kwa kufungua akaunti kwa jina lake facebook ambako hutumia umaarufu wake kutangaza masuala ya mtandao huo.
Asubuhi ya leo (June 27) Adam ameandika kwenye ukurasa wake halisi kulaumu kitendo hicho, “Kuna boya fulani yuko kampuni fulani ya simu amefungua account ya Adam mchomvu Facebook anajiongelesha na kutongozeshana kwa kutumia jina langu. Sasa ajipange yeye na kampuni yake kutoa fidia ya maana tu.. Habari zimfikie tayari hatua za kwanza zimekamilika.â€
Ukifungua akaunti anayoizungumzia Adam ambayo mpaka sasa ina marafiki 735, utakutana na ujumbe mrefu kwenye wall ukiwa na ujumbe kuhusu mtandao huo.
Hata hivyo mtu huyo anaonekana kujihusisha na vitendo vya utapeli kwakuwa anadai anaweza kuwasaidia watu simu zao zitumike kwa kupiga simu kwenda mitandao yote bila malipo kama alivyoandika hapo chini.
“Napenda kuwashukuru wale wote tulio waunganishia Technical program ya tigo mxshare kupiga simu bure kwenda mitandao yote Tanzania, kutuma sms bure kwenda mitandao yote pia kubrowse/downloads bure ktk internet bila malipo yoyote ya vocha.
Bado niko na Technician wa tigo anaehusika na masuala ya Information technology ambae ndie aliegundua hii technical program na ndo anaeunganisha namba ya mtu na kuifanyia Activation mtu anakua na uwezo wa kupiga simu bure kwenda mitandao yote Tanzania.
BADO TUNAENDELEA KUUNGANISHA KAMA UNAHITAJI NI INBOX NAMBA YAKO YA SIMU KISHA NITAMPATIA TECHNICIAN NDANI YA DAKIKA3 ATAIUNGANISHA KISHA UTATHIBITISHA KAMA NI UKWELI PROGRAM HII IPO UTALIPIA Tshs.2500 KUPITIA TIGO PESA TUTAKUUNGANISHA.
KUMBUKA: Hatuchukui pesa yako mpaka tukuunganishe kwanza ktk system uhakikishe kama ni ukweli unaweza kujiunga kisha ndio unalipia kuna serial code ambazo ni mastercode zina generate voucher code za tigo ukishalipia ndio tunakupa zinakua ni namba za siri, ukiziingiza unakua umejiunga.
ONYO: Kama utatuma namba yako tukaiunganisha ukathibitisha ukatakiwa ulipie na ukashindwa kulipia tutaifungia namba yako isifanye kaz tena kwani utakua
umetusumbua. Na kwa anaehisi ni uongo/utapeli plz asicomment, asiniInbox wala asiniulize kitu.â€